MKE WA MTU SUMU,JAMAA AFUMANIWA AKIMLA URODA MKE WA JIRANI YAKE APEWA KIPIGO HADI

Mgoni, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) aliyefumaniwa akiwa na mke wa mtu
AMA kweli duniani kuna vituko! Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Usiku wa tukio, Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwa katika harakati za kusaka matukio katika Jiji la Dar, ndipo ilipokumbana na kelele za watu waliokuwa wakijibizana.
Ilibidi OFM itie timu kwenye nyumba hiyo na kukutana na chanzo kimoja kilichodai kuwa baba mwenye nyumba hiyo anadai kumfumania jirani yake na mkewe kitandani.
Mke wa Bw. Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ akiondolewa eneo la tukio.OFM YATINGA NDANI, YAKUTA MAKUBWA
OFM ilizama ndani ya nyumba hiyo na kukuta purukushani kali ikiendelea, Yusuf akiwa amepandwa na jazba ambapo katika kumkurupusha mgoni huyo alijigonga mahali na kuumia usoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni