Katika
mapenzi kwa asilimia kubwa wanawake huwa wanaona wenyewe ndiyo wanaumia
sana linapotokea suala la usaliti katika mahusiano aliyonayo, lakini
ni wazi kabisa hata wanaume wanaumia sana kwahiyo usifikiri mwanamume
akisalitiwa hawezi kuumia hapana kwani hata yeye ni binadamu inapotokea
ametendwa basi lazima ataumia ijapokuwa maumivu yanatofautiana,,
mwanamke anaweza kuonyesha wazi maumivu anayoyapata lakini mwanamume
akawa anaumia moyoni huku akijionyesha usoni kuwa hajaumia kumbe anaumia
sana. kwahiyo naweza kusema maumivu ya mapenzi hayaangalii mwanamume au
mwanamke inategemea na wewe ulipenda kwa kiasi gani.
maumivu haya hutokana na vitu vingi
ikiwemo kukosa uaminifu, kuachana au kuachika nk,,na kutokana na maumivu
haya hupelekea baadhi ya watu kujuta kupenda,, kuapa kutopenda tena,,na
hata kunywa sumu na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Muhimu ni
kuzingatia suala la mapenzi ya dhati na kuishinda tamaa,,hakuna
anayependa kuumia katika mapenzi kwahiyo basi kama hupendi kuumizwa
usimuumize pia mwenzio,,,kwasababu kuna wengine ni mahodari kuwaliza
wenzi wao kila kukicha. Tubadilike jamani mimi naamini hakuna
kinachoshindikana |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni