Jumanne, 5 Agosti 2014

NAMNA YA KUBADILI MAUMIVU YA MAPENZI KUWA FURAHA

BILA shaka mpenzi msomaji umzima buheri wa afya na muda huu unanifuatilia katika busati letu zuri la mahaba, mahali tunapojuzana na kuelimishana mambo kadha wa kadha yahusuyo mapenzi na uhusiano. Nakukaribisha kwa moyo mkunjufu tuijadili mada yetu ya leo kama inavyojieleza hapo juu.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika zama hizi za sayansi na teknolojia, maumivu ya mapenzi yameongezeka maradufu. Kile tunachoamini kuwa ni maendeleo, kinazidi kuzitesa hisia na nafsi zetu na suala la kutendwa, kuumizwa, kuvunjika mioyo au kusalitiwa, linaonekana kuwa fasheni siku hizi.
Kinachowasumbua wengi ni kushindwa kuelewa nini cha kufanya baada ya kuangukia katika dimbwi la maumivu ya kimapenzi. Hebu kila mtu ajiulize:
Umewahi kukuta SMS ya mapenzi kwenye simu ya mpenzi wako akimtumia mtu mwingine tofauti na wewe? Ulijisikiaje uliposikia mtu mwingine akiitwa majina mazuri ya kimapenzi  na mpenzi wako, pengine kuliko hata yale ambayo huyatumia kwako? Ulichukua uamuzi gani?
Kila mtu ataeleza anavyojua yeye lakini ukweli ni kwamba wengi hawajui kukabiliana na maumivu hata yale yanayosababishwa na maisha ya kawaida. Kwa kuwa maumivu, usaliti, kuvunjika kwa mioyo na uongo katika mapenzi ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa halikwepeki katika zama hizi, jambo la msingi ni kujua nini cha kufanya baada ya kutokewa na dhoruba hizo za kimapenzi.
Hebu msikilize msomaji wangu, Jane wa Ilala Bungoni jijini Dar, alivyokuwa analalama:
“Wiki nzima inaisha sasa, siendi kazini, chakula hakipandi, usingizi sipati wala sitamani kitu chochote, kitu pekee ninachokifanya ni kulia usiku na mchana, naomboleza na kulalama katika kila sekunde inayopotea mpaka natamani kujiua, sioni tena thamani ya kuishi, nayachukia mapenzi, nawachukia wanaume,” alisema Jane huku akilia kutokana na kutendwa na mwandani wake aliyemsaliti kwa kutoka na rafiki yake kipenzi.
Yawezekana Jane hayuko peke yake, wapo wengi ambao wanateswa sana na mapenzi lakini hawana sehemu ya kuyatoa maumivu yao, wanaumia ndani kwa ndani, miili yao inadhoofika kila siku, hawana furaha japokuwa wanapata mahitaji yote muhimu, chanzo kikuu kikiwa ni mapenzi.
Hapo ndipo ninapoona umuhimu wa kila mmoja kujua namna ya kusimama tena pale anapoangushwa na maumivu ya kimapenzi.
Zifuatazo ni mbinu ambazo zitakusaidia kuyabadilisha maumivu yako ya kimapenzi kuwa furaha.

JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU
Hakuna jambo ambalo hutuliza fikra na hisia za mapenzi kama kukubali kumsamehe yule aliyekuudhi kabla hata hajakuomba msamaha na kuamua kusahau yote yaliyotokea. Yawezekana wengi mtasema haiwezekani. Inawezekana na wote waliojaribu mbinu hii walifanikiwa.
Marafiki, lazima kila mmoja aelewe kwamba unapokasirika au kuumizwa, anayeteseka siyo yule aliyekusababishia maumivu bali ni wewe mwenyewe. Hasira au maumivu ya kimapenzi huwa kama moto mkali ambao huitafuna taratibu nafsi ya mhusika.
Ukisamehe maana yake unaupa moyo na akili yako nafasi ya kupata sehemu ya kutulia na kuuzima moto ambao tayari ulishaanza kukolea ndani yako.


Hisia za kuumizwa katika mapenzi kwa mwanaume hazitofautiani na za mwanamke,,wote wanaumia

Katika mapenzi kwa asilimia kubwa wanawake huwa wanaona wenyewe ndiyo wanaumia sana linapotokea  suala la usaliti katika mahusiano aliyonayo, lakini ni wazi kabisa hata wanaume wanaumia sana kwahiyo usifikiri mwanamume akisalitiwa hawezi kuumia hapana kwani hata yeye ni binadamu inapotokea ametendwa basi lazima ataumia ijapokuwa maumivu yanatofautiana,, mwanamke anaweza kuonyesha wazi maumivu anayoyapata lakini mwanamume akawa anaumia moyoni huku akijionyesha usoni kuwa hajaumia kumbe anaumia sana. kwahiyo naweza kusema maumivu ya mapenzi hayaangalii mwanamume au mwanamke inategemea na wewe ulipenda kwa kiasi gani.

maumivu haya hutokana na vitu vingi ikiwemo kukosa uaminifu, kuachana au kuachika nk,,na kutokana na maumivu haya hupelekea baadhi ya watu kujuta kupenda,, kuapa kutopenda tena,,na hata kunywa sumu na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Muhimu ni kuzingatia suala la mapenzi ya dhati na kuishinda tamaa,,hakuna anayependa kuumia katika mapenzi kwahiyo basi kama hupendi kuumizwa usimuumize pia mwenzio,,,kwasababu kuna wengine ni mahodari kuwaliza wenzi wao kila kukicha. Tubadilike jamani mimi naamini hakuna kinachoshindikana

Alhamisi, 26 Juni 2014

UNAFIKIRI NI RAHISI KUMFIKIA HUYU?

  GOOD  POZI  NI CHANZO  CHA MVUTO  WA  KIMAHABA  CHUKUA  HILO  JIFUNZE  KWAKE  UTAWINI  KWA  WAKO  PIA  COZ  KILA  ATAKAPO  KUWAKO  ATAWAZA  POZI  LAKO.

JIFUNZE KUBEMBELEZA ILI MPENZI WAKO AJUE THAMANI YAKO

NI  NJIA  NJEMA  YA  KURUDISHA  HISIA ZA  MPENZI  WAKO  ZILIZOPOTEA  JUU  YAKO,  KUNANJIA  NYINGI ZA KUBEMBELEZA  MPENZI  WAKO  AKUELEWE  LAKINI  HIZI  HAPA  CHINI  NI  BAADHI TU.

1. ONGEA KWA HISIA  KWA  KUTAMBUA  MWENZA WAKO  ANAUCHUNGU  NA WEWE NA NDIYO  MAANA  AMEKOSA  AMANI.

2.MPE  MUDA  WA  YEYE  KUONGEA  YALIYO   KATIKA  MOYO  WAKE  JUU  YAKO NA USIPINGE  HATA  MOJA  KWA  KUFANYA  HIVYO  UTAPUNGUZA  HASIRA  ZAKE.

3. PATA  NAFASI  YA KUMUIMBIA  KAMA  UNAUWEZO  WA  KUIMBA  LAKINI  KAMA  UWEZI  JARIBU  KUATAFUTA WIMBO AMBAO  YEYE  ANAUPENDA NA  UMUWEKEE  KATIKA  CD  ASIKILIZE.

4. MKUMBUSHE  KILICHOWAUNGANISHA  NA  MSAULISHE  KINACHOTAKA  KUWATENGANISHA.

5.  MTIE  MOYO  KWA  KUMUELEZA  KUWA  WEWE   PEKEE  NI  CHAGUO  LAKE NA  MAKOSA  NI  SEHEMU  YA  MAISHA. 

JE UNAIFIKIRIA SIKU YA HARUSI YAKO UNAFIKIRI NINI UKIKIKUMBUKA SIKU HIYO KITAKULIZA?

BAADHI YA WATU    UWA NA MAWAZO MENGI AMBAYO UWAPUNGUZA  MWILI PINDI WAKUMBUKAPO  SIKU ILE MBAYO  WATAKUWA WAKIFUNGA  PINGU YA MAISHA.

TAFITI  ZINAONESHA  WENGI  WAO  UWA NA MSONGAMANO WA MAWAZO KUTOKANA  KUJIULIZA NI VIPI    WANAWEZA  KUWAACHA  WATU WAO WA MWANZO, PIA TAFITI  HII  INASEMA  PIA  BAADHI  YA WATU  UFUNGA  PINGU YA MAISHA  NA  WATU  AMBAO  HAWAJAWACHAGUA  KUTOKA KATIKA  MOYO LAKINI  KUTOKANA  TU  NA UGUMU WA MAISHA  WANAJIKUTA WAKIINGIA HUKO  KANA KWAMBA NI  NJIA YA KUJIKWAMUA KIMAISHA.

SASA BASI  KUTOKANA  NA  HARI  HIYO  NDIYO  MAANA UNAKUTA  WENGINE  WANALIA SANA  UKUMBINI  SIKU YENYEWE YA  HARUSI, WENGI WETU TUKIONA  HARI HIYO  TUNAJIFARIJI NA KUSEMA  ETI WANALIA  KWA FURAHA  LAKINI  UKWELI NI KWAMBA  FURAHA MWENZAKE  NI  TABASAMU  HIVYO  KINACHOWALIZA  PALE NI JINSI  WANAVYOKUMBUKA  HAADI  ZAO  ZA UONGO  WALIZOTOA  KWA  WAPENZI  WAO  WA  UKWELI   SO  TAKE  CARE  UTAPOTEA..SIO  KILA  KILIO  KINAASHIRIA  FURAHA  KINGINE NDO HIVYO  NI   CHA  MAJUTO  KUTOKANA  NA  DHAMBI  ALIYOTENDA   SI  UNAMKUMBUKA   PETRO  ALIPO  MKANA  YESU  MARA  TATU  NAE  BAADA  YA  KUKUKMBUKA  MANENO  YA YESU  ALIANZA  KULIA  HIVYO  NDIVYO  ILIVYO.

WENGINE  UPUNGUA  MWILI  KABISA  SASA  UWA  NAJIULIZA  KAMA  SHEREHE  NI  FURAHA  KWANINI  MTU  AWAZE  NA    KUFIKIA  HATUA  YA  KUPUNGUA  MWILI ULE  NI  UOGA  JUU  YA  WALE  AMBAO  UMEWAIDIA  KUWA  NAO  SASA  UNAJIULIZA  SIJUI  ITAKUAJE  SIKU HIYO  YA  HARUSI  YAKE  IKIFIKA  WAKIMUONA  YUPO  NA  MWINGINE  TOFAUTI  NA  WAO.......... JIULIZE  UPO  KUNDI  GANI  ILI UNENEPE  UKITANGAZIWA  HARUSI  YAKO.


Mwanamke akipenda anapenda kweli hadanganyiki kama ilivyo kwa mwanaume




Ninamshukuru Mungu kwa kunipa afya njema na kuendelea kuniwezesha kundika katika blogger ya mahabati juu ya mahusiano ya kimapenzi.

Na imani nawe msomaji wa blogger hii umzima wa afya na sasa unaendelea na majukumu yako ya ujenzi wa mahusiano yako kwa ajili ya maisha marefu yenye Amani na Upendo wa dhati.

Ni ukweli usiyopingika kuwa mwanamke ni mtu mwenye upendo wa dhati ikilinganishwa na mwanaume ingawa wengi wao sasa wako kimasahi zaidi.

Mwanamke anapoamua kupenda anapenda kwa moyo wake wote na akili zake zote, na wakati wote hutumia kumfikiria Yule anayempenda.

Kwa kufanya vitu mbalimbali mfano kuwanunulia zawadi, za aina mbalimbali, wengi wao hupenda kuwanunulia nguo za ndani, viatu, saa ya ukutani, mkanda wa kiunoni wapenzi wao.

Yote hayo mwanamke anayafanya ili kuimarisha mahusiano zaidi na mpenzi wake, na kumwonyesha kuwa yeye ni wathamani ya juu zaidi kuliko mtu mwingine yoyote.

Wengi wanapofanya hivyo wanakuwa na matarajio tofauti, pengine kupokea zawadi kubwa zaidi kutoka kwa Yule anayempa zawadi, au shukrani za mara kwa mara mfano mke wangu unanifanya nionekane tofauti sana n.k.

Tofauti na hapo wengine wanaambulia patupu hivyo kukata taama ya kuendelea kumfanyia vitu vizuri, na wakati mwingine kujenga hisia za kutokuwa chaguo sahihi kwa mhusika.

Je wewe unampa mke wako zawadi au mume wako zawadi, au unaona ni utoto kupenda zawadi?

Kumbuka kila unachokifanya kina maana kubwa sana katika maisha ya mahusiano kiwe chama ama kibaya, na siku zote mahusiano yenye upendo wa dhati hayaimarishwi na mechi pekee yake.

Kuna mengi ya ziada endelea kufatilia blog hii specialist wa mahaba.